Descriptions
Wananchi wote mnatangaziwa kwamba, tarehe
18 Machi, 2025 Shirika litauza kwa njia ya Mnada wa Hadhara: Gari, samani mbalimbali
za ofisi na vifaa chakavu katika Mikoa ya Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha,
Mwanza,Kagera, Tabora,Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya, Songea,Tanga, Mtwara na
Dar es Salaam kama ifuatavyo:-
1.
Mkoa wa Dar es Salaam: Gari ‘’Toyota Landcruiser, hardtop CC
4164 registration number SU35501’’ la
mwaka 2003 mnada utafanyika katika Ofisi za COASCO Mtaa wa Mazengo Dar es
Salaam
2.
Mikoa
ya Shinyanga, Kilimanjaro na Mtwara:
mnada wa Vifaa mbalimbali vya ofisi katika ofisi za COASCO za mikoa
tajwa.
3.
Mkoa wa Arusha: vifaa vya TEHAMA
mnada utafanyika katika ofisi za COASCO zilizopo jengo la NSSF Arusha
4.
Mkoa wa Mwanza, Morogoro, Iringa, Mbeya, Songea na
Tanga mnada wa Samani mbali mbali za ofisi katika Ofisi za COASCO za Mikoa
tajwa
5.
Mikoa ya Kagera, Tabora na Dodoma mnada wa Samani
za ofisi, vifaa mbalimbali na vifaa vya TEHAMA katika ofisi za COASCO za mikoa
tajwa.
MASHARTI
YA MNADA
i.
Chombo/ kifaa kitauzwa kama kilivyo mahali
kilipo.
ii.
Mnunuzi atalazimika kulipa papo hapo amana (deposit)
isiyopungua asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya chombo/kifaa
alichonunua, na kukamilisha malipo yote yaliyosalia katika muda wa siku kumi na
nne (14) kuanzia tarehe ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili
atakosa haki zote za ununuzi wa chombo/kifaa husika na amana iliyolipwa haitarudishwa.
iii.
Mnunuzi atatakiwa kuondoa/kuchukua chombo
alichonunua katika muda wa siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo.
iv.
Ruhusa ya kuangalia vyombo hivyo itatolewa siku
mbili (2) kabla ya tarehe ya mnada.
v.
Mnada utaanza saa Nne (4.00) asubuhi katika
kila kituo.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
COASCO
S.L.P 761, DODOMA