MKURUGENZI MTENDAJI TANZANIA

HEIDRICK & STRUGGLES

Tanzania 06/11/26 -14/11/26

Descriptions

Mkurugenzi Mtendaji atafanya kazi kwa karibu na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na kanda kuandaa na kutekeleza mkakati dhabiti na endelevu utakao leta kasi ya ukuaji wenye faida, mageuzi ya kidijitali na mifumo ya uendeshaji, kuboresha huduma kwa wateja, kuendeleza ubunifu, kuimarisha uwezo wa taasisi na ushindani sokoni; huku akidumisha utawala bora, usimamizi makini na uzingatiaji kamili wa sheria na kanuni

Majukumu Makuu:

- Kuandaa na kuwasilisha dira ya kimkakati ya Benki, akitafsiri malengo ya kanda na maelekezo ya Bodi kuwa vipaumbele vinavyopimika na mipango ya utekelezaji.

- Kuongoza mageuzi katika Benki, ikiwemo mifumo ya biashara, huduma za kidijitali, data, teknolojia, michakato na namna ya kufanya kazi.

- Kuhakikisha ukuaji endelevu na wenye faida kwa kuimarisha biashara kuu, kuongeza makundi muhimu ya wateja, kuongeza tija na kutumia rasilimali za kifedha kwa ufanisi.

- Kujenga utamaduni unaoweka mteja mbele na kuhakikisha wateja wanapata huduma bora, jumuishi na za kuaminika kupitia njia za huduma za ana kwa ana na kidijitali.

- Kuanzisha na kuendeleza ubunifu unaokidhi mahitaji ya mabadiliko ya soko la Tanzania kupitia bidhaa mpya, mifumo shirikishi, ubia wa kimkakati, na huduma zinazotumia teknolojia.

- Kuunda timu ya uongozi yenye weledi wa hali ya juu, jumuishi, inayowajibika, na kuimarisha mipango ya urithishaji madaraka, uwezo wa kutendajii, na utamaduni wa taasisi.

- Kudumisha mifumo imara ya udhibiti kwa kujumuisha usimamizi wa vihatarishi, uzingatiaji wa sheria, usalama wa mtandao, mwendelezo wa biashara na maandalizi katika mabadiliko ya utekelezaji.

- Kujenga mahusiano ya kuaminika na Benki, Bodi, Kanda, Serikali, wawekezaji, wateja, wafanyakazi, na washirika wa kimkakati.

- Kuimarisha uongozi wenye maadili, utawala bora wa kampuni na utoaji wa huduma za kifedha kwa uwajibikaji, huku akitambua mapema mabadiliko ya kiuchumi, kisheria, ushindani na teknolojia.

Sifa na Vigezo Vinavyohitajika:

- Shahada katika fani inayohusiana na biashara. Sifa za kitaaluma za ACIB au CPA pamoja na shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA) au fani inayohusiana zitakuwa nyongeza.

- Uzoefu wa angalau miaka 15 katika sekta ya benki au huduma za kifedha, ikiwemo uzoefu mkubwa wa uongozi wa juu.

- Uwezo uliothibitishwa wa kuongoza mageuzi ya taasisi, kukuza biashara yenye faida na kusimamia mabadiliko ya kitaasisi katika mazingira yanayosimamiwa na sheria na kanuni.

- Uelewa mpana wa sekta ya benki, huduma za kifedha, kanuni na mazingira ya biashara nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

- Uelewa mzuri wa teknolojia, data na mifumo ya kidijitali, pamoja na uwezo wa kibiashara, usimamizi wa fedha na uongozi wa watu wenye tamaduni tofauti.

- Uwezo wa kufanya kazi na Bodi, kusimamia wadau mbalimbali, kuwasiliana kwa ufanisi, kushawishi na kujadiliana, kwa kuzingatia uadilifu na kufanya maamuzi sahihi.

Maombi ya siri na ya kuaminika, yakiambatanishwa na maelezo kamili ya taaluma/uzoefu wa kazi pamoja na anuani za mawasiliano, yatumwe kwa barua pepe kwenda:[email protected] kabla au ifikapo tarehe 14 Novemba 2026. Tafadhali fahamu kuwa mawasiliano yatafanywa kwa waombaji waliochaguliwa pekee








Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email