TANGAZO LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA MKOA WA DAR

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

30/04/25

Descriptions

Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote
kuwa, Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza
unafanyika katika Mkoa wa
Dar es Salaam kuanzia tarehe 17 hadi tarehe
23 Machi, 2025.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari linafanyika
kwa siku saba kwa kila kituo cha kuandikisha wapiga kura katika Mkoa huu
.




















1.      
SIKU: Uboreshaji unafanyika
kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 17 hadi siku ya Jumapili tarehe 23 Machi, 2025.


2.      
VITUO: Uboreshaji unafanyika
katika vituo vilivyopo katika mitaa.


3.      
MUDA: Vituo vinafunguliwa
saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.


 




 


 



 






                                                              



 



 



 



Uboreshaji unahusisha:
-



1.       
Kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa
Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi ambao hawakuwahi kuandikishwa
hapo awali, na ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 ifikapo tarehe ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.



2.       
Kuboresha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka
eneo moja kwenda eneo lingine la kiuchaguzi (Jimbo au Kata).



3.       
Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura ambao kadi zao
zimepotea au kuharibika.



4.       
Kuboresha au kurekebisha taarifa za wapiga kura.



5.       
Aidha, wapiga kura wanaotaka kuboresha taarifa
zao na wanaohama kituo cha kupigia kura au vyote viwili kwa pamoja, wanaweza
kuanzisha mchakato wa kuboresha kwa kujaza fomu maalum kwa njia ya mtandao
kupitia tovuti ya Tume www.inec.go.tz au anuani ya ovrs.inec.go.tz
kwa kujaza namba ya kitambulisho cha Taifa, namba ya kadi ya mpiga kura, namba
ya simu ya mpiga kura na jina la kata anayokusudia kuhamia, kisha watapokea
ujumbe wenye namba ya utambulisho (token number) ambayo watakwenda nayo katika
kituo cha kuandikisha wapiga kura ili kukamilisha taratibu na kupatiwa kadi ya
mpiga kura.



MAMBO YA KUZINGATIA



·        
Mwananchi
anatakiwa kupanga mstari akiwa kituoni na kusubiri hadi zamu yake ya
kuandikishwa itakapowadia. Watu wenye mahitaji maalumu kama vile wazee,
wagonjwa, watu wenye ulemavu, wajawazito na akina mama wenye watoto wachanga
watakaokwenda nao kituoni watapewa kipaumbele.



·        
Mwananchi
atakapofika katika kituo cha kujiandikisha atachukuliwa alama za vidole vyote
kumi vya mikono na kupigwa picha na kisha kupewa kadi yake mpya hapo hapo
kituoni.



·        
Ni
muhimu kujiandikisha sasa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili uweze
kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na chaguzi zijazo.



·        
Mpiga
kura ambaye ana simu ndogo (maarufu kama kitochi au kiswaswadu) anaweza kuingia
kwenye mfumo wa OVRS kwa kupiga *152*00#, kisha, atachagua namba 8 na
kubonyeza, kisha atachagua namba 2, kisha atabonyeza namba 3 hapo atapata
huduma namba moja hadi nne. Atachagua huduma anayotaka kati ya hizo nne.
Hatimaye, atapata namba ya utambulisho (token number) atakayokwenda nayo
kituoni kukamilisha mchakato wa kupata kadi ya mpiga kura.



·        
Mpiga
kura anaweza pia kuwasiliana moja kwa moja na Maafisa wa Tume waliopo katika
Kituo cha Huduma kwa Mpiga Kura kwa kupiga simu namba 0800112100 bila malipo.



·        
Zoezi
hili halitawahusu wapiga kura ambao
waliandikishwa hapo awali na hawajahama
maeneo yao ya kiuchaguzi na wana kadi zao za mpiga kura.



 



                                                     



KUJIANDISHA KUWA MPIGA
KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA
















 


Saida H. Mohamed


KAIMU MKURUGENZI WA UCHAGUZI


 


 


 


                                          Dk. Wilson Mahera Charles


MKURUGENZI WA UCHAGUZI




 


               Limetolewa tarehe 07 Machi, 2025 na:



 



 


Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email