Descriptions
TANGAZO KWA UMMA
Wizara ya Katiba na Sheria kwa mujibu wa Kanuni za Ithibati
ya Waendesha Maridhiano, Majadiliano, Upatanishi na Usuluhishi, 2021
(Reconciliation, Negotiation, Mediation and Arbitration (Practitioners
Accreditation Regulations, 2021)) imepewa mamlaka ya kusajili Waendesha
Maridhiano, Majadiliano, Upatanishi na Usuluhishi ambao wanakidhi vigezo kwa
mujibu wa Kanuni husika.
Hivyo, Wizara inapenda kuwatangazia Watoa Huduma za Usuluhishi,
Upatanishi, Uendeshaji wa Maridhiano na Majadiliano ambao wamekidhi vigezo
kuwasilisha maombi yao kwa kujaza Fomu ya Maombi Na. TAF1 na kuwasilisha
nyaraka na viambatisho kupitia mfumo kiungo https://mmuu.sheria.go.tz/register.
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana
na Ofisi ya Msajili kupitia [email protected] au Simu Na. 0262160360.
Mwisho wa kupokea maombi
ni tarehe 30 Machi, 2025.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
06 Machi, 2O25