TAARIFA KWA UMMA

MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO

31/03/25

Descriptions



UFUNGUZI WA
MSIMU WA UNUNUZI WA ZAO LA CHOROKO KWA MSIMU 2024/2025 NA UTARATIBU WA USAJILI WA WAKUSANYAJI MAZAO, WAKULIMA
WAKUBWA NA VITUO VYA KUKUSANYIA MAZAO.



 



Msimu wa ununuzi wa zao la choroko kwa mwaka 2024/2025 utafunguliwa rasmi tarehe



29 Januari
2025
. Minada itaanza kufanyika kwenye Mikoa ya Mwanza,
Simiyu, Shinyanga, Mara na Geita. Taarifa zaidi za minada zitatangazwa kwenye
tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii za Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na
Mazao Mchanganyiko (COPRA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).



 



Kwa
mujibu wa Vifungu vya 4(1), na 4(2)(e), (f), (i), (j) vya Sheria ya Usalama wa
Chakula ya Mwaka Sura 249 na Marekebisho yaliyofanywa na Sheria ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko Sura ya 249 , Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao
Mchanganyiko kwa kushirikiana na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala
(WRRB), Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na Soko la Bidhaa
Tanzania (TMX) wametoa Maboresho ya Mwongozo wa Biashara kwa Mazao ya Dengu,
Choroko, Mbaazi, Soya na Ufuta Toleo la 3 – 2025. Mwongozo huo pamoja na mambo
mengine unalenga kulinda ubora wa mazao ya dengu, choroko, mbaazi, soya na
ufuta pamoja na kuongeza wigo wa ushiriki na ushindani kupitia minada. Mwongozo huu unapatikana kwenye
kiunganishi
https://www.copra.go.tz/publications/guidelines.



 



MATAKWA YA USHIRIKI WA WAKUSANYAJI MAZAO
NA WAKULIMA WAKUBWA



 



Mwongozo huo umeainisha
ukusanyaji wa mazao kwa
Njia kuu
mbili
ambapo
mazao yatakusanywa kupitia ushirika
au kupitia
wakusanyaji /wakulima wakubwa
waliosajiliwa na COPRA
. Ili washiriki kwenye biashara ya mazao hayo,
wakusanyaji mazao/wakulima wakubwa, mwongozo umeweka taratibu zifuatazo.



1.    Kuwa na leseni ya biashara;



2.    Kujisajili na COPRA kupitia
kiunganishi cha [email protected]   au maafisa wa COPRA walio katika ofisi za mikoa/kanda
husika



3.    Kutambulisha vituo vya kukusanyia mazao watakavyovitumia kwa COPRA;



4.    Kununua mazao kutoka
kwa wakulima kwa bei isiyopungua
bei elekezi itakayokua
inatangazwa na COPRA kila wiki; na



5.    Kufuata taratibu
zote zilizowekwa kwenye Mwongozo wa Biashara kwa Mazao ya Dengu, Choroko,
Mbaazi, Soya na Ufuta Toleo la 3 – 2025 pamoja na kiambatisho chake Na. 1
vinavyopatikana kupitia kiunganishi cha
https://www.copra.go.tz/publications/guidelines.









URASIMISHAJI WA GHALA



Wakusanyaji wa mazao na
wakulima wakubwa
wataruhusiwa
kurasimisha ghala zao
ili zitumike kama ghala kuu za minada iwapo zitakidhi vigezo vilivyowekwa na Bodi
ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala. Vigezo hivyo vinapatikana kupitia kiunganishi
https://www.wrrb.go.tz/publications/forms.



 



Wakulima
na wadau wengine watakaoendelea kutumia mfumo wa ushirika wataendelea kukusanya
mizigo yao kupitia Vyama vya msingi (AMOCs) na baadae kwenda ghala kuu ambapo
minada itafanyika.



MATAKWA KWA WANUNUZI



Kwa
upande wa wanunuzi watakaoshiriki kwenye minada,
watatakiwa kujisajiliwa
na COPRA
na kuweka kinga ya dhamana kama
ilivyoainishwa katika Maboresho ya Mwongozo wa Biashara kwa Mazao ya Dengu,
Choroko, Mbaazi, Soya na Ufuta Toleo la 3
2025, kupitia Soko la Bidhaa Tanzania TMX kwa utaratibu utakaowekwa na Soko hilo.
Wanunuzi wadogo wanaweza kushiriki
minada kwa kupunguziwa dhamana ili kuchochea
ushiriki wa wazawa kwenye biashara hiyo ya mazao.



 



KUKIDHI MATAKWA YA KUSAFIRISHA MAZAO NJE YA NCHI



Kupitia mwongozo huo
itambulike
kuwa vibali
vya kusafirishia mazao nje ya nchi (Export Permit
) vitakatolewa kwa mizigo
ambayo mauzo yake yamepita kwenye mfumo wa stakabadhi za ghala na minada ya
kidijitali pekee.



 



Kwa muktadha huo, umma
unatangaziwa kuwa ni
marufuku kununua zao la choroko pasipo kufuata
taratibu zilizowekwa katika Mwongozo wa Biashara kwa Mazao ya Dengu, Choroko,
Mbaazi, Soya na Ufuta Toleo la 3 – 2025.
Aidha, msafirishaji wa zao la Choroko atatakiwa kuwa na Hati ya utoaji wa mazao ghalani inayopatikana mara baada ya
mnada kufanyika na malipo kwa wakulima kufanyika.



 



Kwa maelezo ya ziada tafadhali wasiliana nasi kupitia
barua pepe: [email protected].



 



Imetolewa na:



 



 



 



Irene M. Mlola



MKURUGENZI MKUU


Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email