Descriptions
TANGAZO
(UUZAJI WA VIWANJA
VILIVYOPIMWA NA HALMASHAURI)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha anayo
furaha kuutangazia Umma wa Tanzania kuwa Halmashauri inauza Viwanja eneo la
Pangani (Mitamba) katika Mradi unaojulikana kama ‘Kibaha Pangani Project’. Viwanja vitauzwa kuanzia tarehe 29/01/2025
kupitia Mfumo wa TAUSI kwa matumizi yafuatayo:-
Na. | MATUMIZI YA KIWANJA | BEI KWA MITA ZA MRABA |
1 | Makazi | 12,000.00 |
2 | Makazi | 18,000.00 |
3 | Biashara | 19,500.00 |
4 | Makazi | 18,000.00 |
5 | Shule | 16,500.00 |
6 | Hoteli | 21,000.00 |
7 | Migahawa | 21,000.00 |
8 | Viwanda | 30,000.00 |
9 | Huduma | 16,500.00 |
10 | Taasisi | 16,000.00 |
11 | Maeneo | 16,500.00 |
Malipo yote yatafanyika kwa njia ya mfumo wa (Control
number) ambapo malipo ya kwanza ni asilimia (30%) na yatafanyika ndani ya
siku thelathini (30), baada ya malipo ya maombi ya kiwanja, na asilimia sabini
(70%) ya malipo yaliyobaki yafanyike ndani ya siku sitini (60) baada ya malipo
ya awali.
Aidha, kwa watakaoshindwa kukamilisha malipo
kwa wakati, kiwanja kitarejeshwa kwa Mkurugenzi na kuuzwa kwa mwananchi
mwingine bila taarifa yoyote kwa mnunuzi wa awali.
Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi wasiliana na
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Kibaha kwa namba za simu 0738929684, 0738929685
na 0738929683.
WANANCHI WOTE WENYE NIA YA KUNUNUA
VIWANJA MNAKARIBISHWA.
Rogers Jacob Shemwelekwa (PhD)
MKURUGENZI WA MJI
KIBAHA