NAFASI ZA KAZI.

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

Dar es salaam 13/01/20 -23/01/20

DescriptionsTANGAZO
LA NAFASI YA KAZI YA KUKUSANYA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI WILAYA YA TEMEKE,
ILALA NA KINONDONI USHURU WA MLANGONI NA VYOONI UBUNGO, USHURU NA USAFI DRIMP
NA USAFI MAKAO MAKUU, KARIMJEE NA MWANANYAMALAMkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji
la Dar es Salaam anawatangazia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wenye sifa,
nafasi ya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari wilaya ya Temeke, Ilala
na Kinondoni Ushuru wa Mlangoni na Vyooni Ubungo, Ushuru na Usafi Drimp na
Usafi Makao Makuu, Karimjee na Mwananyamala. Kazi hii itakuwa ni ya Mkataba wa
miezi mitatu na mshahara utalipwa kwa kuzingatia Sheria ya Ajira Cap. 300 “Wage
Order” 2013 ambao utakuwa kuanzia Sh.150,000/= kwa mwezi.SIFA
ZA MWOMBAJI:·        
Awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka
18 na umri usiozidi miaka 60·        
Awe na elimu ya darasa la Saba na kuendelea·        
Awe na uwezo wa kutumia “Smart phone” katika
miamala ya malipo·        
Awe na Uzoefu usiopungua miezi sita katika masuala
ya kukusanya Ushuru.·        
Awe mwadilifu na mwaminifu na awe hajawahi kutiwa hatiani
kwa kosa la jinaiMAELEKEZO
YA JUMLA·        
Waombaji waambatishe vivuli vya vyeti vya taaluma
zao pamoja na cheti cha kuzaliwa.·        
Kila barua ya muombaji iambatishwe na picha mbili
ndogo (Passport size) iliyopigwa siku za karibuni, anuani kamili ya makazi
pamoja na namba ya simu.     ·        
Barua ya Maombi iambatishwe na:-     
Barua kutoka kwa wadhamini wawili ambao ni
watumishi wa Serikali zikiwa na picha “Pass port size” ya hivi karibuni, Anuani
kamili ya  makazi, pamoja na namba zao za
simu. -     
Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali
za Mitaa. -     
Wasifu (CV) ·        
Waombaji watakaokuwa “Shortlisted” watajulishwa
kwa njia ya simu tarehe ya usaili. ·        
Barua ya maombi ya kazi iletwe kwa njia ya mkono katika
Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe ya tangazo hili au
kwa njia ya posta kupitia anuani tajwa hapo chini kuanzia saa mbili kamili
(2:00) asubuhi hadi saa 8:00 mchana. 
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 23 Januari, 2020 saa 8:00
mchana. ·        
Kila mwombaji
anapaswa kutaja nafasi ya kazi anayoomba juu ya bahasha ya maombi.Maombi yatumwe kwa Anuani
ifuatayo:-Mkurugenzi
wa Jiji,Halmashauri
ya Jiji,Ukumbi wa
Jiji,1
Barabara ya Morogoro,                                              S.L.P.
9084,          11882 – DAR ES SALAAM Tangazo hili pia linapatikana
kwenye tovuti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo ni www.dcc.go.tz                                                                                    Sipora
J.Liana                                  MKURUGENZI WA
JIJI                      HALMASHAURI YA JIJI LA DAR-ES-SALAAM
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email