WITO YA MAOMBI YA RUZUKU KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KUKUZA NA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI ZA WANAWAKE, WASICHANA NA WATOTO KATIKA MUKTADHA WA UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA

WOMEN FUND TANZANIA

Shinyanga 15/07/21 -31/08/21

DescriptionsI.                   
UTANGULIZIThe
registered Trustee of Women Fund 
Tanzania (WFT-Trust) ni mfuko unaotoa ruzuku kwa maswala ya haki za
wanawake uliosajiliwa mnamo 2008 kama shirika lisilo la kiserikali, mnamo
Septemba 2019 ilisajiliwa upya kama Wadhamini waliosajiliwa wa Mfuko wa
Wanawake Tanzania. Mfuko unazingatia kusaidia utekelezaji wa miradi  ambayo inalenga  kukuza upatikanaji wa haki za wanawake,
wasichana na watoto na  kwa kuchagiza
mabadiliko chanya katika jamii kuhusu haki za wanawake ,wasichana na watoto kwa
kuchangia ujenzi wa TAPO la wanawake kimapinduzi Tanzania na harakati za kuleta
usawa wa kijinsia kwa kuimarisha harakati za wasichana na wanawake nchini kwa
lengo la kukuza  uwezo juu ya maswala na
haki za wanawake, wasichana na  watoto
Tanzania.Katika wito huu , WFT-Trust itatoa ruzuku kwa taasisi, mashirika
ya kijamii na kiraia au vikundi vitakavyokidhi vigezo na masharti ambavyo
vinatekeleza shughuli mbalimbali za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto
chini ya  
Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake
na Watoto ( MTAKUWWA) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Mashirika ya kijamii/ vikundi yenye vigezo yanakaribishwa
kulete maandiko yao ya kuomba ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa afua zilizopo
ndani ya MTAKUWWA na zinazotekelezwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga kupitia  michakato mbalimbali
ya utekelezaji huo.Lengo kuu ya ufadhili huu ni kusaidia kutokomeza ukatili
dhini ya wanawake na Watoto kwa njia shirikisha na jumuishi  kama zilivyoainishwa ndani ya MTAKUWWA.Maswala mengine yanayoweza kuombewa ruzuku ni pamoja na  michakato na mikakati ya kuboresha   utekelezaji wa mpango wa MTAKUWWA ndani ya
halmashauri husika. Mikakati hiyo inaweza kuwa na lengo la kuongeza umiliki na
uwezo wawanajamii kushiriki na kushika hatamu za utekelezaji na kujengea uwezo
wa watendaji wa  Serikali za Mitaa na
wengine (kama vile Asasi za kijamii, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, jamii na
wadau wengine) katika muundo wa MTAKUWWA ili kuongeza ufanisi na kukuza  mifumo shirikishi  ili kuhakikisha ushiriki wa jamii katika
utekelezaji wa  MTAKUWWA. II.                 
WFT-TRUST
INATARAJIA RUZUKU ZITAKAZOTOLEWA ZIENDE KUTEKELEZA MIKAKATI IFUATAYO.    ·        
Kuchagiza utekelezaji
wa masuala ya jamii yanayohusiana na MTAKUWWA pamoja na kuhakikisha kuwa kuna uhusiano
wa moja kwa moja  kati ya tatizo
linaloshughulikiwa, mikakati ya utekelezaji pamoja na  matokeo yanayopimika kutokana nautekelezaji wa
mradi husika. ·        
Kuonesha
uendelevu wa shughuli zilizofadhiliwa,ubunifu pamoja na jinsi ya kuonesha ni
jinsi gani kuna uwezekano wa shughuli hizo kutumika kama mfano kwa maeneo
mengine kwa kiwangu cha juu zaidi. ·        
Kuonesha
mchango wake katika jitihada za ujenzi wa TAPO la pamoja baina ya watetezi wa
haki za wanawake na watoto na pia katika kupigania kutokomeza aina zote za
uklatili dhidi ya wanawake na watoto kwa pamoja na haswa kwa kuimarisha
muingiliano baina ya mashirika na asasi hizo za utetezi.katika  (harakati/ vuguvugu la pamoja)  kwa lengo la kutengeneza / kuimarisha
mitandao na majukwaa ya kuleta nguvu ya pamoja·        
Kujenga
ari ya umiliki na uwezo wa kuimarisha umiliki wa mchakato wa MTAKUWWA na miundo
yake ya utekelezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ·        
Kukuza
mikakati na jitihada zenye kuimarisha ujenzi wa TAPO la wanawake na Watoto. III.               
VIGEZO MUHIMU KWA
WAOMBAJI WA RUZUKU ·        
Mashirika
ya kijamii / Vikundi vya kijamii vinavyotambulika kisheria na wanaotekeleza
shughuli zake ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.·        
Mashirika ya kijamii/ vikundi vya kijamii  ambavyo vimekuwa wakitekeleza shughuli za
MTAKUWWA  katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga.·        
Mashirika ya kijamii/ vikundi vya kijamii  yenye mtazamo 
kama wa WFT - Trust katika kuondoa taratibu za kibaguzi na kuleta usawa
wa kijinsia ili kuondoa udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na Watoto, na
ambao shughuli zao zinalandana na maudhui ya shirika la WFT-Trust.  ·        
Taasisi nyingine
zinazotambulika kisheria zenye uhalali na fursa za kutekeleza na / au
kusimamia   utekelezaji wa MTAKUWWA ndani
ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.  IV.              
MADIRISHA YA
UFADHILI DIRISHA DOGO LA UFADHILI ·        
Kiwango cha
ruzuku inayotolewa (TSH 10,000,000 – TSH 15,000,000)·        
Muda wa kutekeleza
mradi/shughuli ( miezi 0 -  3 )·        
Sifa – Ruzuku
katika dirisha hili zinaweza kuombwa na Mashirika / Taasisi zinazotekeleza na
kusimamia mikakati ya muda mfupi ya 
utekelezaji wa MTAKUWWA.  DIRISHA LA KATI LA UFADHILI·        
Kiwango chauzuku
inayotolewa ni kati ya  ( TSH 16,000,000-
TSH 50,000,000)·        
Muda wa kutekeleza
mradi kuanzia miezi 6 hadi mwaka mmoja·        
Sifa - Ruzuku
katika dirisha hili zinaweza kuombwa na Mashirika / Taasisi zinazotekeleza na
kusimamia mikakati ya muda wa kati katika utekelezaji wa MTAKUWWA

 


JINSI
YA KUOMBA  RUZUKU


 


Waombaji wa
ruzuku wafuate hatua zifuatazo:


 


1.       Kuwasilisha Andiko la Mradi (Iisilozidi
kurasa 5-7) likielezea mradi pendekezwa utakaotelezwa


 


2.       Andiko la mradi litumwe na viambatanisho
vifuatavyo:


·        
Nakala ya cheti cha usajili cha
shirika/kikundi


·        
Nakala ya katiba ya shirika/
kikundi


·        
Taarifa ya karibuni ya akaunti ya
benki ya shirika/ kikundi


 


3.     
 
Maombi
yote yatumwe kwa kutumia fomu ya muongozo wa maombi ya ruzuku inayopatikana
katika tovuti ya WFT-Trust: www.wft.or.tz . Fomu pia
zinapatikana katika ofisi za WFT-Trust zilizopo Jengo jipya la NSSF MAFAO
House barabara ya mwanza, Ghorofa ya kwanza ( muda wa kazi)


 


Maombi
yatumwe kwa barua barua pepe:
grants@wftrust.or.tz     kichwa
cha habari kisomeke “NPA VAWC SHINYANGA “


Ama kwa sanduku la barua


Mkurugenzi
Mtendaji, WFT-Trust,


S. L.
P 79235
, Dar es Salaam


 Ama ziletwe kwa mkono katika ofisi za
WFT-Trust zilizopo Jengo jipya la NSSF MAFAO House
barabara ya mwanza, Ghorofa ya
kwanza ( muda wa kazi)

 


Kwa maelezo Zaidi unaweza
kuwasiliana na WFT-Trust kwa nambari : +255 753 912130.


 


4.       Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26 /07/
2021, saa kumi na moja jioni


 


* Waombaji
wote watajulishwa kuhusu kupokelewa kwa maombi yao na kuhusu hatua
inayofuata katika mchakato wa kupata ruzuku kabla ya tarehe 31 /08/ 2021.


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 


 

         

       
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email