Descriptions
TAARIFA KWA UMMA
(Imetolewa chini ya kifungu Na.19 cha sheria ya
Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Sura ya 414 ya
Sheria za Tanzania na Kanuni Na. 20 (4) ya Kanuni za Mafuta Biashara ya Jumla,
Uhifadhi, Rejareja na Matumizi binafsi (Gazeti la Serikali Toleo Na. 150 la 2022)
TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi la kubadili umiliki wa leseni
na jina la kituo cha mafuta kama ifuatavyo: -
Jina
la awali la kituo: Asood
Petroleum Company Limited-Chamanzi
Mbagala
Nambari
ya Leseni: PRL-2020-390
Mahali
Kituo kilipo: Kiwanja Namba. 1,
Kitalu “J’’Eneo la Chamanzi, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam
Jina linalopendekezwa: Allyen Company Limited
Mmiliki wa awali: Asood Petroleum Company Limited
Mmiliki mpya: Allyen Company Limited
Mtu yeyote mwenye maoni au
pingamizi dhidi ya mabadiliko ya umiliki na majina ya leseni tajwa hapo juu,
afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani iliyotajwa hapa
chini ndani ya siku kumi na nne toka tarehe ya tangazo hili.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
EWURA