TANGAZO-MAHAKAMA YA TANZANIA

MAHAKAMA YA TANZANIA

28/02/23

Descriptions                                                 
    
TANGAZOMahakama
ya Tanzania inawatangazia Wananchi wote kuwa Wiki ya Sheria itaadhimishwa
nchini kote kuanzia tarehe 22 Januari, 2023 hadi tarehe 29 Januari, 2023.          Wiki
hii itaadhimishwa Kitaifa jijini Dodoma katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’
ambapo kutakuwa na Maonesho ya Shughuli mbalimbali za kimahakama. Wiki ya
Sheria inatarajiwa kuzinduliwa kwa Matembezi Maalum yatakayofanyika Siku ya
Jumapili tarehe 22 Januari, 2023 Saa 12:00 asubuhi. Matembezi hayo yataanzia
Viwanja vya Kituo Jumuishi Cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma na kuishia Viwanja vya ‘Nyerere
Square’. Matembezi hayo yataongozwa na Mhe.Dkt. Phillip Isdori Mpango, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wadau
watakaoshiriki kwenye Maonesho ni Chama cha Mawakili  Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu, Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania na
wengine.Ndugu
Mwananchi, endapo una shida yoyote ya Mambo ya Kisheria, maoni au mapendekezo ya
Uboreshaji wa Huduma za Mahakama tafadhali fika kwenye Viwanja vya Maonesho ili
upate ushauri na huduma mbalimbali za Kisheria kutoka kwa Majaji, Wasajili, Mahakimu,
Watendaji na Wadau wengine wa Mahakama watakaokuwa kwenye Viwanja vya Maonesho.Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yatahitimishwa na Kilele
cha Siku ya Sheria nchini tarehe 01 Februari, 2023, kuanzia saa 03:00 Asubuhi katika
Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ni Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kauli mbiu ya Wiki na Siku ya Sheria 2023
ni; ‘Umuhimu wa utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Usuluhishi katika kukuza uchumi
endelevu: Wajibu wa Mahakama na Wadau.’Wote mnakaribishwa.Imetolewa
na;                      Artemony Vincent,MKUU WA KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA
MAWASILIANO,MAHAKAMA YA TANZANIA. 
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email