TAARIFA YA TAHADHARI KWA WANAHISA SWALA OIL & GAS (TANZANIA) PLC (DSE: SWALA)

SWALA OIL & GAS (TANZANIA) PLC (DSE: SWALA)

30/09/21

DescriptionsTAARIFA YA
TAHADHARI KWA WANAHISASWALA
OIL & GAS (TANZANIA) PLC (DSE: SWALA)(Imesajiliwa
katika Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania) (“Swala” au “Kampuni”)Swala Oil & Gas (Tanzania)
plc ("Swala" au "Kampuni") inashauri wanahisa kwamba
Kampuni imeanza majadiliano juu ya kubadilisha utaratibu wa malipo ya madeni  inayodai. Tarehe 29 Desemba 2017
Kampuni ilitoa dhamana ya bondi za daraja la juu la kwanza (A1) kwenda kwa kampuni
ya Panafrican Energy Corporation (PAEC) ili kupata riba ya usawa wa asilimia
7.93%. PAEC inamiliki asilimia 100% ya Panafrican Energy Tanzania Limited
(“PAET”) Kampuni ambayo ndio inasimamia mradi wa gesi ya Songo Songo hapa Tanzania. Mnamo  tarehe 22 Januari, 2021 mdhamana halali wa
bondi alifikiria kuondoa maslahi yake kwenye mradi kufuatia kipindi cha miaka
miwili ambacho PAEC ilishindwa kutoa mapato yoyote kwa wanahisa. Kushindwa huko
kulitokana na sababu ya uwekezaji mpya wa mapato katika mradi wa Songo Songo,
Ulipaji wa haki na faida ya kupata gesi kwa shirika la maendeleo ya petroli
(TPDC) na majukumu ya ulipaji wa ushuru wa PAET. Kama ilivyoshauriwa, tarehe
7/6/2021, mdhamana halali wa bondi aliuza maslahi yake kwa Kampuni ya watu binafsi
wenye uzoefu mkubwa katika masoko yanayochipukia (“Mnunuzi”).
Uamuzi wa mmiliki wa zamani wa kuuza maslahi yake, ulileta
fursa kwa mnunuzi kupata bondi kwa msingi ambao unaonesha kwa karibu zaidi
utabiri wa kifedha wa PAEC na PAET hadi mwisho wa matumizi ya leseni ya Songo
Songo mnamo mwaka 2026. Tarehe hiyo hiyo Kampuni ilielezea kuwa ni mwanzo wa utaratibu
wa mazungumzo ya ulipaji wa madeni  (“Mapendekezo
ya malipo”). Swala na washauri wake
wamekuwa na mazungumzo mengi na Mnunuzi na baadhi ya wanahisa wake ili
kufanikisha utaratibu wa malipo uliopendekezwa.
Wakati
bado majadiliano ya namna ya kufanya malipo hayajakamilika, imepelekea
kuanishwa kuwa matokeo yake yataleta mabadiliko kwenye mahesabu ya biashara ya
kampuni, hali inayomlazimu mkaguzi wa nje wa mahesabu ya kampuni kuandaa maoni
kuhusiana na mahesabu ya kampuni yanayoishia tarehe 31 Disemba 2020. Kwa mujibu wa kanuni za Soko
la Hisa la Dare es Salaam, Kampuni inahitajika kuchapisha na kutangaza kwa umma
taarifa za hesabu za mwaka zilizokaguliwa ndani ya miezi sita (6) ya mwisho wa
mwaka wa kifedha. Kwasababu tajwa hapo juu, Kampuni haikuwa katika nafasi ya
kuchapisha na kuatangaza kwa umma taarifa zake za kifedha zilizokaguliwa za
mwaka 2020 ilipofika tarehe 30/6/2021 na bado haina uwezo wa kufanya hivyo
kwani wakaguzi wake wa mahesabu wa kujitegemea BDO, hawajaridhia kutokana na
majadiliano juu ya kubadilisha ulipaji wa madeni ambayo bado yanaendelea. Kampuni na mnunuzi wanatumia
njia bora zaidi ya kuweza kumaliza majadiliano hayo ili kuweza kuwapa wakaguzi
wa nje ushahidi wa kutosha kuwaruhusu kuhitimisha madai ya kampuni
yaliyopo  na hivyo kuweza kutoa maoni
sahihi ya ukaguzi kuhusiana na taarifa za kifedha kwa mwaka uliomalizika 31
Disemba 2020. Mchakato huu unatarajia kutokea kabla ya tarehe 15 Oktoba 2021. Bado hakujawa na uhakika
kwamba makubaliano ya mapendekezo ya malipo yatafanyika au, wala masharti
ambayo malipo yaliyopendekezwa yanaweza kufanywa. Wasomaji wanaonywa kuwa Swala
au Mnunuzi anaweza kuamua kutoendelea na utaratibu wa Mapendekezo ya malipo na
Wanahisa wanashauriwa ipasavyo kuwa waangalifu wanaposhughulika na usalama wa
hisa zao za Swala. Kwa Habari zaidi tafadhali wasiliana na:Swala
Oil & Gas (Tanzania) plcBi. Christina EugeneChristina.eugene@swalaoilandgas.comwww.swalaoilandgas.com  Taarifa za wakati ujao Utoaji huu wa habari
unajumuisha "taarifa za wakati ujao" na "habari za wakati ujao"
(“kwa pamoja taarifa za kutazama wakati ujao”) kwa maana ya sheria ya dhamani
inayotumika, pamoja na kuanza kwa malipo yaliyopendekezwa, masharti yake pamoja
na kukamilika kwa mafanikio ya malipo. Taarifa hizi zinategemea matarajio ya
sasa ya usimamizi, imani, mawazo na makadirio na sio dhamana ya muda, matokeo
ya baadaye au utendaji. Taarifa za wakati ujao zinajumuisha umakini na
uangalifu na kutokuwa na uhakika na sababu zingine ambazo zinaweza kusababisha
matokeo halisi kutofautina na yale yaliyooneshwa katika taarifa za wakati ujao
na kwa hivyo, wasomaji wanaonywa wasiweke tegemeo lisilofaa kwa taarifa zozote za
wakati ujao. Angalizo hili na kutokuwa na uhakika ni pamoja na uwezo wa kuingia
mikataba dhahiri kwa makubaliano ya kifedha yaliyopendekezwa kwa masharti
yanayokubalika na Swala na kwa wakati unaofaa, uwezo wa kupata idhini zote
zinazohitajika za kisheria na kupata idhini ya wanahisa kwa wakati unaofaa. Kuhusu Swala: Swala ni kampuni ya kwanza ya
Mafuta na Gesi iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Afrika Mashariki na
umiliki muhimu wa ndani. Swala inamiliki mali zake katika bonde la ufa la
Africa Mashariki yenye ukubwa zaidi ya 14,000 
Km2 pamoja na riba ya asilimia 7.93% katika shirika la nishati la PAE
Panafrican. Uvumbuzi mpya umetangazwa na washiriki wa tasnia katika leseni
kadhaa kama bilionea  Albert Graben alifanikiwa
sana na Tullow Oil katika upande wa kushoto wa mashariki ya bonde la ufa. Swala
ina mpango wa maendeleo katika biashara ili kuweza kuendelea kukuza uwepo wake
katika  hydrocarbon ya Afrika Mashariki
na ulimwenguni.       
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email