KUWASILISHA FOMU ZA MREJESHO (ARF) KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 KWA MTANDAO

BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI

30/09/21

DescriptionsBodi inapenda kuwataarifu Makandarasi wote nchini kwamba
muda wa kuwasilisha fomu za mrejesho (ARF) kwa mwaka wa fedha 2020/21 kwa njia
ya mtandao umewadia na mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 30 Septemba 2021. Bodi
haitatuma fomu za mrejesho kwenda kwa makandarasi kwa njia ya posta wala fomu
hizo  hazitapatikana kwa kupakua kutoka
katika tovuti ya Bodi.  Ili kuupata mfumo wa kukuwezesha kujaza fomu ya mrejesho
mtandaoni, ingiza“URL” https://mis.crbtz.org
au fuata “link” kupitia tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz(ARF 2020/21) ili kujisajili kuwa mtumiaji wa mfumo. Kupitia
mfumo wa mtandao, mtumiaji atachagua ‘‘Register’’ ili kusajili akaunti yake ya
kutumia mfumo. Mtumiaji atajaza taarifa zote zitakiwazo na kuchagua “Submit”.
Utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” vitatumwa kwa
mtumiaji kupitia barua pepe iliyoingizwa na mtumiaji kipindi cha kujisajili
mtandaoni.   Ili kujaza fomu ya mrejesho mtandaoni, mtumiaji wa mtandao
aliyejisajili ataingia mtandaoni kupitia “URL” au “link” kwa kuingiza
utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” kama
ilivyoelekezwa awali. Kupitia ukurasa utakaojitokeza, mtumiaji atabofya “ARF”
katika “Create new ARF”’ na kuingiza taarifa zote zitakiwazo na kisha kubofya
“Submit” baada ya kukamilisha.  Mtumiaji atalazimika kurekebisha mapungufu hadi fomu
itakapokubalika na mfumo. Uwasilishaji wa fomu hizi mtandaoni ni lazima ufanywe
na Mkurugenzi Mkuu, “Managing Director” au Mkurugenzi wa Ufundi, “Technical Director”.  Maelekezo haya ya jinsi ya kuufikia mfumo na kujaza fomu
mtandaoni pia yanapatikana katika tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz.  Mwisho wa kuwasilisha fomu za mrejesho kwa mwaka wa fedha
2020/21 kwa mtandao ni tarehe 30 Septemba 2021.   R. NKORIMSAJILI
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email