SERIKALI YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA KUINGIZA MBOLEA KWA WINGI NCHINI

YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KILIMO MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA TANZANIA

06/08/21

DescriptionsKatika kuhakikisha
upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei ya ushindani, kwa msimu wa kilimo
wa 2021/22,  Waziri wa Kilimo  Mh. Profesa 
Adolf  Mkenda, Kupitia kifungu Na.
7(4) cha Kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja ameruhusu wafanyabiashara, makampuni
 kuingiza mbolea nchini bila kupitia
zabuni za ununuzi wa mbolea kwa pamoja.Wafanyabiashara  wanahimizwa kuingiza mbolea kwa wingi  ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nchi
jirani ambazo hununua mbolea kutoka Tanzania. Serekali  inatarajia kuwa ruhusa hii ya soko huria
itasaidia kuongeza upatikanaji, kukuza ushindani  na kudhibiti mfumuko wa bei za mbolea.     Dkt. Stephan E. NgailoMKURUGENZI MTENDAJI


Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email