MWALIKO KWA WATAZAMAJI WA NDANI WA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

31/01/20

DescriptionsTume ya Taifa ya Uchaguzi iko kwenye mchakato wa
maandalizi ya kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika
Mwezi Oktoba, 2020.Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kualika
na kusajili Watazamaji wa Uchaguzi wanaotaka kutazama Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Kupitia tangazo hili, Tume inapenda kualika maombi kutoka Taasisi/Asasi mbalimbali
nchini ambazo zinahitaji kutazama Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika mwezi
Oktoba, 2020.Taasisi/Asasi zenye nia ya kutazama Uchaguzi Mkuu zinatakiwa
kuwasilisha maombi yao katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Foreign Affairs House, Mtaa wa Shabani Robert/Garden
Avenue
kuanzia tarehe 28 Novemba, 2019 na mwisho wa kupokea maombi hayo itakuwa
ni tarehe 31 Januari, 2020.Aidha, maombi hayo pia yanaweza kutumwa Tume
kupitia anuani ya Posta ifuatayo;Tume ya Taifa ya UchaguziForeign
Affairs House,Mtaa
wa Shabani Robert/ Garden Avenue,S.L.P
10923DAR
ES SALAAM Barua ya maombi pamoja na mambo mengine itatakiwa kuainisha
mambo yafuatayo:-(i)                        
Anuani
kamili ya Taasisi husika;(ii)                         
Mahali/sehemu
ambapo Taasisi husika inafanya kazi;(iii)           
Shughuli
ambazo zinafanywa na Taasisi husika kwa mujibu wa hati ya Usajili;(iv)           
Sehemu
ambazo Asasi/Taasisi inataka kufanya zoezi hilo la Utazamaji;(v)             
Idadi
ya watu ambao Taasisi/Asasi itawatumia katika zoezi hilo pamoja na taarifa zao;(vi)           
Kutaja
majina na namba za simu za viongozi wa Taasisi/Asasi husika kama yalivyoandikwa
katika hati za usajili wa Taasisi/Asasi;(vii)         
Ikiwa Taasisi/Asasi inahusisha
Watendaji wa Kimataifa, wawili lazima wawe Watanzania.(viii)       
Kuambatisha
Nakala/kivuli cha hati ya Usajili wa Taasisi/Asasi husika; na(ix)                       
Kuambatisha
Nakala/kivuli cha Katiba ya Taasisi/Asasi husika.Tume baada ya kupokea barua za maombi itazitaarifu
Taasisi/Asasi husika iwapo zimekubaliwa au kukataliwa.                                                    Imetolewa na; MKURUGENZI
WA UCHAGUZITAREHE:
........................
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email