TAARIFA YA KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA ISHIRINI (20) WA WANAHISA WA BENKI YA MUCOBA KUTOKA TAREHE 23/11/2019 NA KUWA TAREHE 30/11/2019

MUCOBA BANK PLC

30/11/19

DescriptionsTaarifa inatolewa kwa wanahisa
kwamba, Mkutano Mkuu wa ishirini wa Wanahisa uliotakiwa kufanyika siku ya Jumamosi
tarehe 23 mwezi wa Novemba 2019 sasa umesogezwa mbele na kuwa tarehe 30/11/2019
katika ukumbi wa MAM HALL –uliopo Mafinga
Mjini
kuanzia saa tatu kamili asubuhi. Sababu
kuu ya kusogezwa mbele tarehe ya mkutano huu ni 
kupisha uchaguzi mkuu wa Kitaifa wa Serikali za Mitaa ambapo kila
mwananchi ana haki ya kushiriki.Uongozi wa benki unaomba radhi kwa usumbufu
wowote uliojitokeza Ajenda za Mkutano zitabakia kuwa
zile zile zilizotangazwa awali  ambazo ni:  1. Kufungua Mkutano
 2. Kuthibitisha Akidi
  ya Wajumbe
 3. Kuchagua Mwenyekiti
  wa Mkutano
 4. Kuridhia ajenda
  za Mkutano
 5. Kuthibitisha Muhtasari
  wa kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa uliofanyika tarehe
  25.08.2018
 6. Kupokea,kujadili
  na kuridhia utekelezaji wa yatokanayo na Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa
  uliofanyika tarehe  25.08.2018
 7. Kupokea na
  kujadili taarifa ya Mwenyekiti wa bodi 
  ya Wakurugenzi  ya Mwaka 2018
 8. Kupokea na
  kujadili taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za Mwaka ulioshia tarehe
  31.12.2018
 9. kujadili
  pendekezo la kuongeza mtaji  wa Benki
 10. Kupokea na
  kujadili mapendekezo ya Mkaguzi huru wa hesabu za benki kwa mwaka 2018
 11. Kuchagua na kuthibitisha
  Wajumbe wapya wa Bodi
 12. Kupokea na kujadili gawio
  kwa mwaka ulioishia tarehe 31.12.2018
 13. Kupokea na
  kuidhinisha pendekezo la Malipo ya wajumbe wa Bodi
 14. Kuwasilisha
  taarifa kuhusu mashauri yahusuyo Benki
 15. Kupokea na
  kuidhinisha uteuzi wa wakaguzi wa nje wa hesabu  kwa mwaka 2019
 16. Kufunga Mkutano.


 Notisi hii imetolewa leo tarehe
04/11/ 2019 Mambo ya kuzingatia 1. Mwanahisa anayetarajia
  kuhudhuria Mkutano huu atatakiwa kufanya hivyo kwa gharama zake mwenyewe;
  na atatakiwa
 2. Iwapo Mwanahisa
  anayeruhusiwa kuhudhuria Mkutano na kupiga kura, atashindwa kwa sababu
  zozote zile kuhudhuria Mkutano, ataruhusiwa kuchagua Mwakilishi kuhudhuria
  na kupiga kura kwa niaba yake kwa kufuata na kuzingatia taratibu na sheria
  za Kampuni.


  1. Nakala za Makabrasha ya
  Mkutano zitapatikana pia kwenye ofisi yetu kuu iliyopo Mafinga- Iringa.


 KWA
AGIZO LA BODI YA WAKURUGENZIPHILIP  RAYMOND PHANUEL
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email