2.0 MABORESHO YA MFUMO WA SOKO LA KAHAWA NGAZI YA AWALI (FARMGATE MARKET)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BODI YA KAHAWA TANZANIA

29/11/19

DescriptionsJAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIABODI YA
KAHAWA TANZANIA (Imeanzishwa
kwa Sheria Namba 23 ya Mwaka 2001 na Marekebisho yaSheria
ya Bodi za Mazao ya Mwaka 2009) TAARIFA KWA UMMA  1.0.         
UTANGULIZI: Serikali katika
kuboresha usimamizi wa mazao ya kipaumbele ilifanya maboresho kwenye mfumo wa
masoko ya kahawa ambapo kuanzia msimu wa mauzo ya kahawa 2018/2019 kahawa yote
inakusanywa na kuuzwa na Vyama Vya Ushirika. Vyama Vya Ushirika vya Msingi na
Vyama Vikuu vina jukumu la kuikusanya na kuipeleka kahawa kwenye viwanda vya
kutayarisha kahawa ngazi ya pili na baadaye kwenye masoko ya kahawa. Katika utekelezaji
wa mfumo huu kwa msimu wa kwanza kumejitokeza changamoto ambazo zinahitaji
mfumo huu kufanyiwa maboresho ili kuongeza ufanisi na kufikia malengo
yaliyokusudiwa na Serikali. Moja ya changamoto ni kuchelewa kwa malipo ya
wakulima kutokana na kahawa kuchelewa kupelekwa sokoni, kuongezeka kwa mnyororo
wa thamani wa kahawa unaosababisha malipo kwa wakulima kuchukua muda mrefu na
na upungufu wa mitaji (Liquidity). Aidha, kuna ushindani mdogo wa bei katika
soko la awali. 2.0     
MABORESHO YA MFUMO WA SOKO LA KAHAWA NGAZI YA AWALI (FARMGATE MARKET) Kutokana na
changamoto hiyo, Serikali kupitia Bodi ya Kahawa Tanzania kwa mujibu wa Kanuni
Na. 63 ya Kanuni za Kahawa za Mwaka 2013, inatoa maelekezo ya nyongeza kufuatia
Mwongozo wa Maboresho ya Taratibu za Mfumo wa Masoko ya Kahawa uliotolewa kwa
umma tarehe 28 Juni, 2019. Maboresho haya yanalenga kuboresha utaratibu wa soko
la kahawa ngazi ya awali kwa lengo la kutatua changamoto ya bei ya mkulima na
kuongeza ufanisi katika Sekta ya Kahawa.2.1.     
UTARATIBU WA SOKO LA AWALI Wanunuzi binafsi
wataruhusiwa kununua kahawa kwa wakulima moja kwa moja kupitia Vyama Vya
Ushirika vilivyoko katika maeneo yao. Kahawa itakayonunuliwa katika soko hili
ni ile ambayo tayari imepitia utayarishaji ngazi ya awali
(Dry cherries & Parchment) kwa kufuata utaratibu wa ununuzi wa kahawa katika soko la awali kwa mujibu
wa sheria. Wanunuzi wa kahawa katika soko hili watatakiwa kuwa na leseni ya
ununuzi wa kahawa vijijini zinazotolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa mujibu
wa Sheria (
Parchment Buyers License and Dry
Cherry Buyers License
). Mnunuzi wa kahawa
atakayehitaji kununua kiasi chochote cha kahawa atapaswa kuingia makubaliano na
chama cha ushirika husika. Pamoja na mambo mengine, makubaliano hayo
yataonyesha bei ya kahawa itakayotolewa na mnunuzi wa kahawa. Vilevile,
makubaliano hayo yatapitishwa na Ofisi ya Mrajisi wa Ushirika na Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika na kusajiliwa na Bodi ya Kahawa. Mnunuzi wa kahawa
atakuwa huru kuipeleka kahawa kwenye kiwanda cha ukoboaji ngazi ya pili (
Secondary Processing) alichokiainisha
kwenye maombi ya Leseni ya Ununuzi wa Kahawa na kuiuza katika soko la mnada au
kwa utaratibu wa soko la moja kwa moja. ANGALIZO: Kahawa ambazo tayari
zipo kwenye utaratibu wa mikopo na taasisi za fedha na watoa huduma wengine
hazitahusika katika utaratibu huu na endapo mnunuzi yeyote atapenda kununua
atalazimika kurejesha kwanza fedha za mkopo ili aweze kununua kahawa hiyo. 2.2.     
BEI YA KAHAWA Wanunuzi
watakaonunua kahawa katika soko hili watatoa bei ya kununulia kahawa ambayo si
chini ya bei zifuatazo; 

AINA YA KAHAWABEI KWA KILO YA KAHAWA
GHAFIRobusta
maganda (Dry Cherry)1,500Arabika Ngumu
(Dry Arabica Cherry)1,600Arabika Laini
(Parchment)4,000
 Bei hizo atalipwa mkulima kupitia chama chake cha
ushirika na Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru wa Halmashauri. Imetolewa
na  MKURUGENZI MKUUBODI YA KAHAWA TANZANIAS. L. P 732MOSHI.
Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email